TANA RIVER CVE ACTION PLAN EXECUTIVE SUMMARY IN KISWAHILI
UFUPISHO WA MPANGO MKAKATI WA KAUNTI YA TANA-RIVER KATIKA KUZUIA NA KUPAMBANA NA ITIKADI NA MISIMAMO MIKALI 2019-2023
1.0 UTANGULIZI
Mpango mikakati wa kuzuia na kapambana na itikadi na misimamo mikali katika kaunti ya Tana River ni juhudi za shirika la KECOSCE zilizotekelezwa katika muda wa miaka miwili baada ya majadiliano ya kina kati ya serikali na mashirika ya kijamii.Ni mpango uliofadhiliwa na shirika la USAID,chini ya mradi wa kuiboresha jamii kuzuia kuendelezwa kwa itikadi na misimamo mikali (SCORE) na kwa ushirikiano na shirika la UKAID’s chini ya mradi wa hazina ya usalama na udhabiti wa kaunti. Mpango huu unapendekeza mikakati itakayotekelezwa kwa ushirikiano ili kuhini usajili wa watu katika makundi yenye misimamo na kujiunga na makundi ya kigaidi.
Mpango mikakati huu umepangwa katika nguzo 11,zinazolenga kupambana na dalili za itikadi na misimamo mikali katika kaunti ya Tana River.
Utekelezaji wa mapendekezo haya katika muda wa miaka mitano,utakuwa msingi wa kutimia kwa mpango wa kitaifa wa kupambana na itikadi na misimamo mikali katika kaunti ya Tana River.
Kiini cha mapendekezo haya ni ushirikiano baina ya serikali na mashirika ya kijamii chini ya uongozi wa gavana na kamishena wa kaunti utahitajika.Kamati tekelezi(Jopo la utekelezaji) la mpango mikakati huu litaratibu na kushirikisha wadau ili kuhakikisha utekelezaji wa mpango huu. Hatua hii itawezesha kujumuishwa kwa kila mkaazi kama njia moja wapo ya kupambana na itikadi na misimamo mikali.Itikadi na misimamo mikali ni ile hali ya mtu ama watu kuwa na imani kali kupita kiasi katika dini ama siasa, na kumfanya mfuasi kuwa tayari ama kuunga mkono hatua ya kusababisha vurugu kutokana na usadikifu.